• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wadau waiomba EWURA kuwasaidia Wananchi wanaotumia Chupa za Maji kusafirisha Mafuta

Posted on: February 22nd, 2019

Wadau wa Nishati na Maji mkoani Simiyu wameiomba Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuangalia namna ya kuwasaidia wananchi wanaotumia chupa za maji kusafirisha mafuta vijijini na badala yake watafute njia mbadala ili kuepusha majanga ya moto na uchakachuaji wa nishati hiyo.

Wadau hao wametoa ushauri huo katika mkutano baina ya watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) uliolenga  kuelimisha wadau Mkoani Simiyu kuhusu majukumu ya Mamlaka hiyo, uliofanyika Mjini Bariadi Februari 21, 2019.

Wakizungumza katika mkutano huo wamesema kutokuwepo vyombo maalum vya ubebaji wa mafuta ya taa , petroli na diseli ni Moja ya tatizo kubwa, hivyo ni vema (EWURA) ikaja na njia mbadala ya kuwawezesha wananchi kusafirisha kwa usalama nishati hiyo.

“Tunaomba EWURA isaidie kuja na namna bora, vifaa vidogo vitakavyouzwa kwa bei rahisi ili wananchi waweze kusafirisha na kuhifadhi kwa urahisi kwa sababu yanawasaidia sana” amesema Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto Wilaya ya Bariadi, Maulo Kigahe.

Katika hatua nyingine wadau hao wamezungumzia suala la urasimu katika kuunganishwa kwa umeme kwa wananchi katika baadhi ya ofisi za Mameneja wa TANESCO  na kuomba EWURA ione namna ya kuwasaidia wananchi wasaidiwe kupata huduma kwa wakati.

“ Kuna wananchi wakitaka  kuunganishiwa umeme majumbani kwao wanadaiwa pesa mara shilingi laki tano, mara milioni moja hivi EWURA wanayajua matatizo haya? Tukizingatia kuwa umeme ni moja ya huduma muhimu kwa mwananchi tubadilike maana hata kule vijijini tulikozaliwa tunahitaji umeme” alisema Mkuu wa  Gereza Wilaya ya Bariadi, Kajungu Massami.

Naye Saibogi Mwandu mwananchi kutoka Bariadi amesema ni vema wafanyabiashara wadogo hususani wanaouza mafuta ya petroli kwenye chupa wakapewa elimu ya namna ya kutunza mafuta hayo kwani wengi wao wamekuwa wakitunza bidhaa hiyo ndani.

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Mawasiliano (EWURA) makao makuu Wilfred Mwakalosi amesema EWURA katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imeshabuni mwongozo utakaosaidia wawekezaji wa vijijini kuwekeza kwenye vituo vya gharama nafuu.

Akifunga mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe Festo Kiswaga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewataka wadau wote kuwa mabalozi wazuri wa EWURA ili wasaidie kufikisha elimu waliyoipata katika maeneo yao.

Awali akifungua mkutano huo, Kiswaga amesema Mkoa wa Simiyu umejipanga katika utekelezaji wa Sera ya Viwanda kwa kujenga viwanda ikiwemo kiwanda cha vifaa tiba, kiwanda cha chaki na vingine ambavyo vitahitaji huduma za nishati na maji , hivyo ameiomba EWURA kushirikiana na Taasisi zinazohusika na utoaji wa huduma hizo katika kuhakikisha zinatolewa katika viwango vinavyokidhi mahitaji ili Mkoa uweze kufikia malengo yake katika uzalishaji katika viwanda.

MWISHO.

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/02/wadau-waiomba-ewura-kuwasaidia-wananchi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda, Naibu Waziri TAMISEMI Dkt Dugange Wanogesha RCC Simiyu

    December 16, 2020
  • TANROADS Simiyu Kutumia Bilioni 11.4 Ujenzi wa Barabara na Madaraja

    December 16, 2020
  • Viongozi, Wananchi na Wadau Simiyu Watakiwa Kushirikiana Kukamilisha Ujenzi wa Madarasa

    December 13, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa