• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Ombi la Wananchi Simiyu la Eneo la Malisho Lapokelewa na Serikali, Laahidiwa Kufikishwa kwa Rais Magufuli

Posted on: February 20th, 2019

Mwenyekiti wa Timu  maalum ya mawaziri wanane ya kupitia maeneo yenye migogoro kati ya wananchi na maeneo ya Hifadhi, Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo na Makazi Mhe. Wiliam Lukuvi amepokea ombi la wananchi wa wilaya tatu za mkoa wa Simiyu wanaoishi katika vijiji vinavyopakana na Pori la Akiba la Maswa la kupewa eneo lenye urefu wa kilometa kumi, kwa ajili ya malisho na kuahidi kulifikisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua zaidi.

Mhe. Lukuvi ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Vijiji vinavyopakana na pori la akiba la Maswa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mji mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu.

Awali akijibu baadhi ya kero zilizowasilishwa na Mwananchi wa Wilaya ya Meatu, Bw. Deusdedith Martin  Waziri Lukuvi amesema timu hiyo imezisikia kero hizo na akaahidi kuwasilisha taarifa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kubainisha kuwa taarifa rasmi ya majibu ya kero zao itatolewa.

Aidha, Waziri  Lukuvi amewahakikishia wananchi kuwa zoezi la kupima eneo la mita 500 kutoka kwenye mpaka wa Pori la Akiba la Maswa kuelekea kwenye vijiji vinavyopakana na Pori hilo (Buffer zone)  katika Wilaya za Meatu, Itilima na Maswa limesimamishwa mpaka litakapotolewa maelekezo.

“Hapa kulikuwa na zoezi la kupima mita 500 kutoka kwenye mpaka wa Pori la Akiba la Maswa kuingia kwa wananchi, maana yake ni kwamba kuna wananchi wengi na vijiji vingi vingeathirika ili vipishe ‘buffer zone’, ingawa ni kwa mujibu wa sheria lakini ‘buffer zone’ ile ingekula maeneo ya vijiji kwa hiyo zoezi hilo limesimamishwa”

“Zoezi hili limesimamishwa kwa mujibu wa maelekezo ya Mhe Rais baada ya kuona watu wengi maskini ambao walipaswa kupisha maeneo ya hifadhi;...... vile vile kuanzia sasa zoezi lolote la kutambua mipaka litakalofanywa na watu wa Maliasili ni lazima liwe shirikishi” alisema Waziri Lukuvi.

Awali akiwasilisha taarifa kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Meatu, Bw. Deusdedit Martin aliomba Timu ya Mawaziri wanane kuwasaidia katika kutatua changamoto ya ubadilishaji wa mpaka kati ya Pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyopakana, Uvamizi wa tembo katika mashamba na makazi ya watu na kukatazwa kwa wananchi kulima katika eneo la mita 60 kutoka kwenye kingo za mito.

Kwa upande wake Waziri wa Maji, Mhe. Prof.  Makame Mbarawa amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Simiyu upatikanaji wa uhakika wa maji kupitia mradi mkubwa wa Ziwa Victoria, ambapo amesema kwa sasa mradi upo  katika hatua ya kumtafuta mkandarasi

Naye  Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe.Omari Mgumba akieleza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inatoa viatiifu kwa wakulima ambapo amesema hadi sasa zaidi ya chupa milioni saba zimeshasambazwa kwa wakulima katika mikoa inayolima pamba hapa nchini.

Timu ya Mawaziri wanane inayoongozwa na Waziri Lukuvi pia inajumuisha mawaziri kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Maliasili na Utalii, Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Maji na Manaibu Waziri kutoka Wizara ya Kilimo na Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/02/ombi-la-wananchi-simiyu-la-eneo-la.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • Wanafunzi Simiyu Waomba Kambi za Kitaaluma Ziwe Endelevu

    April 14, 2021
  • Wastaafu Wawaasa Watumishi Kufanya Kazi kwa Kujituma

    April 14, 2021
  • Malalamiko ya Wachimbaji, Wenye Mashamba Mgodi wa Bulumbaka Bariadi Yashughulikiwe: RAS Simiyu

    April 08, 2021
  • Viongozi Simiyu Waaswa Kutumia Busara Badala ya Nguvu

    March 14, 2021
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa