Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio zake leo Mkoani Simiyu na kukabidhiwa katika Mkoa wa Mara, ambapo miradi 33 kati 34 sawa na asilimia 97 ya miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri zote sita imekubaliwa na kuzinduliwa, kukaguliwa, kuonwa na kuwekewa mawe ya msingi.
Akitoa taarifa kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru mkoani Mara, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema ni mradi mmoja tu wa maji ambao umeonekana kuwa na kasoro ambapo amebainisha kuwa kasoro hizo zitafanyiwa kazi na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2019 atapata taarifa mapema iwezekanavyo ya namna zilivyofanyiwa kazi.
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali amewapongeza viongozi na wananchi Mkoani Simiyu, huku akibainisha kuwa tangu mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 zizinduliwe rasmi Mkoani Songwe, Simiyu ni mkoa wa Tisa lakini umeonekana kuwa mkoa nambari moja kwa namna ulivyolitekeleza jukumu hili.
Aidha, amesema yeye pamoja na wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa wengine katika kipindi cha siku sita walizokaa Simiyu wamebaini kuwepo kwa umoja, ushirikiano na kuheshimiana miongoni mwa wananchi, watumishi na viongozi mambo ambayo ni ya msingi katika maendeleo.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:https://simiyuregion.blogspot.com/2019/05/mwenge-wa-uhuru-wamaliza-mbio-zake.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa