• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Malipo ya Wakulima wa Pamba Simiyu Kufanyika Kielektroniki

Posted on: October 3rd, 2019

Malipo ya Wakulima wa zao la Pamba Mkoani Simiyu, katika msimu ujao yanatarajiwa kufanyika kwa mfumo wa kielektroniki kupitia huduma ya T-PESA ya Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL).

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Mkutano wa Wadau wa Pamba uliowahusisha viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, wataalam wa kilimo, viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS), kwa lengo la kujadili juu ya malipo ya wakulima wa zao hilo kupitia huduma ya T-PESA uliofanyika Oktoba 02, 2019  mjini Bariadi.

Mtaka amesema kuwa sambamba na mfumo wa ulipaji wa fedha za wakulima wa pamba kwa njia ya Kielekroniki taarifa zote za kilimo zitapatikana kwa njia hiyo huku akiongeza kuwa mfumo huo utasaidia kuondokana na hasara katika vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) iliyokuwa inasababishwa na baadhi ya viongozi wasio waaminifu.

“Tumewaleta hapa TTCL tunataka tufanye digital farming(kilimo kidigitali) malipo ya pamba, mambo yote ya pamba na kilimo kwa ujumla yawe kwenye kiganja chako kwa sababu leo hakuna nyumba ambayo haina simu; ni vizuri elimu hii viongozi wa AMCOS muifikishe kwa wakulima ili wawe  na uelewa wa pamoja,” alisema Mtaka.

Akizungumza katika Mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Waziri Kinamba amesema mfumo huo mpya utaanza kutumika katika msimu ujao na utawasaidia wakulima kupata fedha zao kwa usalama, urahisi, kwa wakati na kupunguza matumizi yasiyofaa.

“Lengo letu ni kutoa suluhu ya matatizo mbalimbali yanayojitokeza katika vyama vya msingi vya ushirika kama upotevu wa fedha, uporaji na tunaamini wakulima wakipata pesa zao kidigitali itaondoa changamoto hizo na kuwafanya wakulima kuwa na maisha bora kutokana na uchumi utakaoboreka baada ya mauzo watakayofanya kupitia TTCL PESA,” alisema Kindamba.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ushirika Mkoa (SIMCU), Emmanuel Mwelele amesema kuwa mfumo huu ni mzuri na unalenga kwasaidia wakulima kupata fedha zao kwa usalama na akaahidi kuwa viongozi wa chama hicho watatoa elimu kwa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) ili wakulima wote wawe na uelewa wa pamoja.

Hadi sasa mkoa wa Simiyu una wakulima wa pamba wapatao 314,000 na matarajio ya uzalishaji katika msimu wa mwaka huu yalikuwa ni kufikia kilo milioni 180, ambapo hadi sasa jumla ya kilo milioni 148 zimekusanywa kutoka kwa wakulima kupitia vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS).

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/10/malipo-ya-wakulima-wa-pamba-simiyu_3.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • Kila Mtumishi Itilima Ashiriki Kikamilifu Ukusanyaji Wa Mapato: RAS Simiyu

    February 27, 2021
  • RAS Simiyu Awaasa Viongozi wa Dini, Waganga wa Tiba Asili Kushiriki Kupunguza Vifo vya Wajawazito na Watoto

    February 27, 2021
  • Watu Wenye Ulemavu Watakiwa Kuchangamkia Fursa ya Mikopo ya Asilimia Mbili Kutoka Halmashauri

    January 30, 2021
  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa