• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Maafisa Maendeleo ya Jamii waaswa Kutumia Taaluma yao Kuleta Mabadiliko katika Jamii

Posted on: April 12th, 2017

Maafisa Maendeleo ya Jamii wametakiwa kutumia taaluma yao kuleta mabadiliko katika jamii kwa kubaini fursa mbalimbali zinazoweza kuwaletea wananchi maendeleo katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini katika ufunguzi wa Kikao cha Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Kanda ya Ziwa kilichofanyika Mjini Bariadi.

Sagini amesema kutokana na taaluma yao Maafisa Maendeleo ya Jamii wanaweza kuwasiliana na jamii na kueleweka kwa urahisi zaidi hivyo watumie fursa hiyo kuwashauri wananchi na vikundi mbalimbali kufanya shughuli zinazoweza kuwaingizia kipato ili waondokane na umaskini.

Amesema wananchi wengi wanafanya shughuli mbalimbali lakini wanakosa elimu, uwezeshwaji na taarifa sahihi za masoko na mitaji  ili kuendeleza shughuli wanazofanya, hivyo akawataka kutimiza wajibu wao katika kuelimisha na kuihamasisha jamii kuunda vikundi  hususani vijana na wanawake ili watambuliwe na kuwezeshwa.

Akizungumzia namna Maafisa Maendeleo ya Jamii katika mkoa wa Simiyu walivyoshiriki katika maendeleo ya Simiyu ya Viwanda, amesema walibaini vikundi vya vijana katika maeneo yao na kubuni uanzishwaji wa viwanda vidogo wiwili ambavyo ni Kiwanda cha kutengeneza Chaki (Maswa) na Kiwanda cha kusindika maziwa(Meatu).

“Maafisa Maendeleo ya Jamii wangu walishirikiana na Wakurugenzi wakabaini fursa mbalimbali  kwenye maeneo yao na vikundi vya vijana ambavyo kwa sasa vinaendesha miradi ya viwanda kwa kushirikiana na Halmashauri, kiwanda cha kutengeneza chaki kilichopo Maswa na kingine cha kusindika maziwa kipo Wilaya ya Meatu” alisema.

“Nawashauri na ninyi mfanye vitu vitakavyofanya mtambuliwe, fanyeni yale yanayogusa shida za wananchi, mkifanya hivyo wananchi watawatambua, viongozi watawatambua na Mungu pia atawatambua” alisema.

Mwenyekiti aliyeongoza kikao cha Maafisa Maendeleo ya Jamii Kanda ya Ziwa ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya Serengeti, Ndg.Wambura Sunday amesema maafisa hao wanafanya jitihada mbalimbali katika maeneo yao na wanaiomba Serikali iwasaidie kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utendaji wao.

Aidha, Wambura amesema kikao chao kimependekeza uanzishwaji wa Chama cha wana taaluma ya Maendeleo ya Jamii Tanzania ili kudhibiti ubora na viwango vya utoaji huduma katika Taaluma ya Maendeleo ya Jamii.

Kikao cha Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri na Mikoa ya Kanda ya Ziwa  kimefanyika kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kupashana habari juu ya masuala mbalimbali ya utendaji wa sekta hiyo na vikao kama hivi vimefanyika katika kanda nyingine sita za Tanzania katika maeneo tofauti.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • Naibu Waziri Silinde Aridhishwa Ujenzi wa Bwalo, Madarasa Sekondari ya Anthony Mtaka Busega

    March 06, 2021
  • A NaibuWaziri Silinde Aridhishwa Ujenzi wa Bwalo, Madarasa Sekondari ya Anthony Mtaka Busega

    March 06, 2021
  • Naibu Waziri Silinde Atoa Miezi Miwili Bariadi, Itilima Kukamilisha Mabweni

    March 05, 2021
  • Bilioni 75 Kujenga Kituo Cha Kupozea Umeme Simiyu

    March 04, 2021
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa