• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wataalam wa Afya Watakiwa kutoa Elimu ya Matumizi Sahihi ya Dawa

Posted on: July 6th, 2017

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017 Ndg, Amour  Hamad Amour amewataka watalaam wa afya kutoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa kwa wananchi ili kuepuka madhara mbalimbali kiafya.

Ndg.Amour ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Duka la Dawa katika Hospitali ya Somanda Mjini Bariadi.

Amesema baadhi ya watu wamekuwa wakitumia dawa kwa mazoea pasipo kufuata maelekezo ya madaktari na wauguzi hali ambayo ni hatari kwa afya  zao.

“ Wapo watu wanatumia dawa kiholela na kuathiri kinga ya mwili, inafika kipindi dawa zinawaathiri moja kwa moja hata wanapotakiwa kuzitumia kutibu maradhi waliyonayo haziwasaidii, wapeni elimu wananchi watumie dawa kulingana na maelekezo ya wataalam”

Aidha, amewataka madaktari na wauguzi kutoa huduma stahiki kwa wananchi kupitia duka hilo kwa kuwauzia dawa kwa bei elekezi na kuhakikisha dawa zinapatikana wakati wote,  ili wanapoandikiwa dawa na kuikosa hospitali, vituo vya afya na zahanati wazipate katika duka hilo.

Kwa upande wake mmoja wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Ndg.Fredrick Ndahani ameipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto kwa jitihada za kuhakikisha kuwa kila Hospitali ya Mkoa na Wilaya inakuwa na Duka la dawa la Bohari  ya Dawa ya Taifa(MSD), ambayo yatawawezesha wananchi kupata dawa zenye ubora wa hali ya juu na kwa bei nafuu.

 Sanjali na hilo Ndahani ametoa wito kwa wanachi wote kujenga utamaduni wa kuangalia tarehe ya mwisho wa matumizi ya dawa(expire date) kabla ya kutumia ili wasitumie dawa zilizokwisha muda wake.

Akiwasilisha taarifa ya mradi wa duka la dawa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Mganga mkuu wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Dkt.Akilimali Mponzemenya amesema lengo la kujenga duka hilo ni  kuwezesha upatikanaji wa dawa zilizothibitishwa na Mamlaka ya Dawa kwa urahisi na kwa bei nafuu zaidi kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi katika maeneo tofauti, ametoa wito kwa wananchi wote kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi bidii  na kulinda rasilimali za nchi hii.

Mwenge wa Uhuru unaendele na Mbio zake Mkoani na leo upo katika Halmashauri ya Mji Bariadi, ambapo umeweka mawe ya msingi, kufungua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya Afya, Elimu , Maji, Ujenzi na Maendeleo ya Jamii na jumla ya miradi 6 imepitiwa pamoja na klabu ya wapinga rushwa kufunguliwa katika Shule ya Sekondari Bariadi.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda, Naibu Waziri TAMISEMI Dkt Dugange Wanogesha RCC Simiyu

    December 16, 2020
  • TANROADS Simiyu Kutumia Bilioni 11.4 Ujenzi wa Barabara na Madaraja

    December 16, 2020
  • Viongozi, Wananchi na Wadau Simiyu Watakiwa Kushirikiana Kukamilisha Ujenzi wa Madarasa

    December 13, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa