• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Kamati ya Siasa ya CCM Simiyu Yaeleza Kuridhishwa na Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa 2018

Posted on: July 30th, 2018

Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM ) mkoa wa Simiyu imeelezea kuridhishwa na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima (Nanenane) yatakayofanyika Kitaifa mwaka 2018 Mkoani humo, katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Mhe. Enock Yakobo, mara baada ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa huo, kutembelea Uwanja wa Nanenane Nyakabindi na kukagua baadhi ya mabanda ya maonesho ya Nanenane uwanjani hapo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Mhe. Enock Yakobo, amesema kamati hiyo imeridhishwa na maandalizi hayo na kuwaomba wananchi kujitokeza ili kupata elimu kuhusiana na teknolojia ya kisasa ya kilimo na ufugaji.

“ Maandalizi yako vizuri, wananchi watakaofika hapa nina uhakika watafaidika na elimu ya ufugaji,  kilimo, matumizi ya zana bora za kilimo, wataona bidhaa mbalimbali za viwanda zinazolishwa  lakini pia watapata motisha wa kwenda kufanya vizuri kwenye maeneo yao” alisema Mhe. Enoc

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi la Kujenga Taifa,  SUMA JKT Meja Peter Sebyiga amesema Jeshi hilo limejiaandaa vizuri katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi , hivyo akatoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kujifunza.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema  maandalizi ya nane nane yamekamilika kwa asilimia 100, ambapo amebainisha kuwa Taasisi, Mashirika na makampuni yatakayoonesha teknolojia za kilimo, mifugo na uvuvi, wasindikaji na waongeza thamani katika mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi wameshafika kwa wingi.

Aidha, amewakaribisha wananchi wote hususani wa Mkoa wa Simiyu kufika katika maonesho hayo huku akibainisha kuwa kufika kwa wananchi katika maonesho hayo kutakidhi malengo ya mkoa  ya kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi kupitia mafunzo watakayoyapata katika maonesho hayo.

Ameongeza kuwa kupitia Nanenane hii wananchi watapata fursa ya kuona kwa macho teknolojia mbalimbali zitakazowahamisha kutoka kwenye kile walichonacho katika maisha yao ya kila siku kuja kwenye teknolojia za kisasa.

“Matarajio yangu ni kwamba Nanenane hii itakuwa ni mahali sahihi kwa wananchi wa Simiyu kama wenyeji kubadilisha masha yao kutoka katika kufanya shughuli zao za kilimo, mifugo na uvuvi kwa mazoea kwenda kuzifanya shughuli hizo kisasa zaidi” alisema Mtaka.

Kauli mbiu ya Nanenane mwaka 2018 ni “WEKEZA KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA MAENDELEO YA VIWANDA”

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/07/kamati-ya-siasa-ya-ccm-simiyu-yaeleza.html


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • Kilo 145,000 za Choroko Zauzwa Mnada wa Kwanza Simiyu

    March 02, 2021
  • Mrajisi Atakiwa Kutoa Vibali kwa Wafanyabiashara Kusafirisha Choroko

    March 01, 2021
  • Choroko Zilizonunuliwa Nje ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani Zipelekwe Ghala Kuu: RAS Simiyu

    February 28, 2021
  • Kila Mtumishi Itilima Ashiriki Kikamilifu Ukusanyaji Wa Mapato: RAS Simiyu

    February 27, 2021
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa