• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

JKT Yaahidi Kujenga Majengo ya Kudumu Uwanja wa Nanenane Simiyu

Posted on: July 26th, 2018

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT)  Meja Jenerali Martin Busungu ameahidi kuwa Jeshi hilo  litajenga Majengo ya kudumu katika Uwanja wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane Kanda ya Ziwa  Mashariki wa Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu, ili kuendelea kutoa elimu ya teknolojia mbalimbali za  kilimo na ufugaji kwa wakulima, wafugaji na wavuvi.

Meja Jenerali Busungu ameyasema hayo wakati alipotembelea eneo la JKT lililopo Uwanja wa  Nanenane Nyakabindi kwa lengo la kujionea maandalizi hayo yanayofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa.

Busungu amesema baada ya Nanenane wataanza ujenzi wa majengo ya kudumu ili wakulima, wafugaji na wavuvi  wanufaike na teknolojia ya kilimo kwa muda wote.

“Mkuu wa mkoa ametupa mkakati wao kuwa kila baada ya miezi mitatu kutakuwa na maonesho katika uwanja huu, tunaahidi kujenga majengo ya kudumu hapa na maonesho yajayo miezi mitatu inayofuata wananchi watarajie kupata vitu vizuri kutoka JKT, maana JKT ni kisima cha kila kitu” alisema Meja Jenerali Busungu.

“ Katika maonesho haya watarajie kuona teknolojia mbalimbali za kilimo, ufugaji, uvuvi pia watarajie kuona bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na JKT zikiwemo bidhaa za kilimo, viwanda na kwa ndugu zangu Wanyantuzu wataona mbuzi na kondoo wa maziwa na wataona kuwa si ng’ombe tu wanaotoa maziwa” alisisitiza Meja Jenerali Busungu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru JKT  kwa kazi kubwa ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane waliyoifanya, huku akibainisha kuwa uwepo wa JKT  utasaidia kuwabaadilisha vijana wa Simiyu kwa kuwa watapata fursa ya kujifunza teknolojia mbalimbali.

“ Tunawashukuru sana JKT kwa kutuamini na tunajua kuwepo JKT kutasadia kuwabadilisha vijana wa hapa kwa kuwa kuna vijana wanamaliza darasa la saba au kidato cha nne hawana pa kushika na sisi tuna vikundi vingi vya vijana , tuko tayari kuleta vikundi vyetu vya vijana kuja kujifunza hapa” alisisitiza Mtaka.

Naye Mbunge wa Itilima amesema maonesho hayo yatawasaidia wananchi kupata elimu itakayowawezesha kufanya uzalishaji wenye tija ikiwemo ufugaji wa kisasa na kilimo bora.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/07/jkt-yaahidi-kujenga-majengo-ya-kudumu.html

Matangazo

  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Tangazo la Nafasi za kazi, Chama Kikuu cha Ushirika Simiyu (SIMCU) October 17, 2018
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Kidato cha kwanza mwaka 2019 Simiyu December 18, 2018
  • Uhamisho wa Watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Januari-Machi, 2018 March 26, 2018
  • Fungua

Habari Mpya

  • Wafungwa 136 Waachiwa Huru Simiyu Kufuatia Msamaha wa Rais, Waahidi kuwa Raia Wema

    December 10, 2019
  • Wanafunzi 18,306 Wachaguliwa Kidato cha Kwanza Mwaka 2019 Simiyu

    December 06, 2019
  • Viongozi wa Umma Watakiwa Kuepuka Mgongano wa Kimaslahi Katika Maamuzi Wanayofanya

    December 04, 2019
  • Serikali Yawafichua Watoto 16,000 Wenye Ulemavu Waliofichwa na Kuwaandikisha Shule

    December 03, 2019
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa