• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Halmashauri Zakaribisha Wawekezaji Kuwekeza Kwenye Viwanja Vinavyopimwa

Posted on: August 21st, 2018

Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Halmashauri ya Wilaya ya Busega na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu zinawakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kuwekeza kwenye jumla ya viwanja 3758 vilivyopimwa na vinavyotarajiwa kupimwa kwa nyakati tofauti.

Hayo yamebainishwa na Viongozi wa Halmashauri hizo katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru Viongozi,watumishi na wadau mbalimbali waliofanikisha, kilichofanyika Agosti 20, Mjini Bariadi.

Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo amesema Halmashauri yake inatarajia kupima viwanja 758 katika eneo la Maperani, huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko akibainisha kuwa Halmashauri hiyo kuanzia Septemba Mosi, 2018 itaanza kupima viwanja 1000 katika eneo la Malampaka.

Naye Mkurugenzi wa Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Kabuko amesema Halmashauri hiyo imeanza kupima viwanja 2000 Agosti 20, 2018  katika eneo ambalo liko umbali wa chini ya kilomita moja kutoka Ziwa Victoria, pia imetenga ekari zaidi ya 2000 kwa ajili ya uwekezaji na akasisitiza kuwa ardhi itatolewa bure kwa wawekezaji watakaotaka kujenga viwanda.

Viongozi hao wametoa wito kwa wafanyabiashara, wawekezaji wa ndani na nje ya mkoa wa Simiyu,Taasisi, mashirika, makampuni na wananchi kujitokeza kununua viwanja hivyo kwa ajili ya kuviendeleza kwa uwekezaji na kubainisha kuwa maeneo yote yanayotarajiwa kupimwa Bariadi, Maswa na Busega ni ya kimkakati katika uwekezaji.

"Kuanzia tarehe 01 Septemba, tutaanza kupima viwanja 1000 katika eneo la Malampaka Maswa, ni eneo la kimkakati katika uwekezaji kwa sababu patapitiwa na Standard Gauge(Reli ya Kisasa) na patajengwa dry port (bandari kavu), nitoe wito kwa wafanyabiashara kuja kununua viwanja Malampaka kwa ajili ya kufanya uwekezaji mbalimbali; kwa wale wawekezaji watakaotaka kujenga viwanda sisi Maswa tutatoa ardhi bure" alisema Dkt. Sagamiko.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa Wafanyabiashara wa Mkoa huo kuwekeza katika Ujenzi wa Hoteli, Nyumba za kulala wageni na kumbi za mikutano hususani katika Eneo la Uwanja wa Nanenane Nyabindi na maeneo mengine, ili kukabiliana na changamoto ya malazi kwa kuwa Simiyu imepewa heshima ya kuwa Mwenyeji wa Maonesho ya Nanenane kwa miaka mitatu mfululizo.

Amesema pamoja na kuwa mwenyeji wa Maonesho Nanenane Kitaifa yapo matukio mengine yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu, ikiwa ni pamoja na Maonesho ya SIDO Kitaifa Oktoba 2018, Maadhimisho ya Kimataifa ya siku ya watu wenye Ulemavu Desemba 2018, Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya hapa nchini mwaka 2019 na mengine mengi yatafuata baada ya hapo hivyo maandalizi ni muhimu..

Amesema Serikali mkoani humo kupitia Halmashauri zake imedhamiria kuwekeza katika ujenzi wa sehemu za malazi lakini inaendelea kuweka msukumo kwa wafanyabishara kuwekeza si tu katika ujenzi wa nyumba za kulala wageni na hoteli, bali katika ujenzi wa vituo vya mafuta, maeneo ya utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za chakula na huduma za kibenki.

Mmoja wa Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu Bw. Malongo Midimu amesema wako tayari kuwekeza mkoani hapa na akaomba Serikali pamoja Taasisi za Kifedha zikiwemo Benki kuondoa vikwazo na urasimu pale wanapohitaji masuala hayo

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo ametoa wito kwa Wafanyabiashara kujipanga katika uwekezaji kwa kuwa Simiyu inabadilika na inaendelea kufunguka ambapo amebainisha kuwa kukamilika kwa Ujenzi wa miundombinu kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa eneo la Igegu wilaya ya Bariadi, barabara ya Maswa-Bariadi kutachangia ukuaji wa uchumi wa Mkoa.

Kikao cha Tathmini ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018, Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, kiliwahusisha Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali ngazi ya Mkoa na Wilaya, Watumishi na Wadau mbalimbali wakiwemo Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu kikiwa na lengo la kushukuru na kutambua mchango wa wadau wote muhimu waliofanikisha maonesho hayo.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/08/halmashauri-zakaribisha-wawekezaji.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • Kila Mtumishi Itilima Ashiriki Kikamilifu Ukusanyaji Wa Mapato: RAS Simiyu

    February 27, 2021
  • RAS Simiyu Awaasa Viongozi wa Dini, Waganga wa Tiba Asili Kushiriki Kupunguza Vifo vya Wajawazito na Watoto

    February 27, 2021
  • Watu Wenye Ulemavu Watakiwa Kuchangamkia Fursa ya Mikopo ya Asilimia Mbili Kutoka Halmashauri

    January 30, 2021
  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa