• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Dkt Gwajima Aagiza Mikoa Yote Nchini Kufanya Ukaguzi wa Vituo yya Afya

Posted on: August 11th, 2020

" Mikoa yote fanyeni ukaguzi katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya kama mlivyofanya kwa vichache na mkagundua matatizo mengi kwenye usimamizi wa mfumo wa ugavi na ikaonekana bayana kwamba mkiongeza usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi mnaziba mianya ya watu fulani ambao wanadhani vituo hivyo ni shamba la bibi,"

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima.katika kikao kazi kilichowahusisha Viongozi mbalimbali, wataalam wa afya mkoa wa Simiyu pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Afya, katika kikao kazi kilichofanyika Agosti 11, 2020 Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Aidha, Dkt. Gwajima amesema taarifa ya ukaguzi huo unapaswa kufanyika kila robo inapokamilika na taarifa iwasilishwe wiki mbili baadaye na kufafanua kuwa taarifa ya awali itapokelewa Oktoba 15 baada ya kukamilika kwa robo ya kwanza ya mwezi Juni-Septemba mwaka 2020/2021.

Ameongeza kuwa ukaguzi huo ufanywe na wataalam waliobobea kwenye masuala ya ukaguzi wakiwemo wakaguzi wa ndani na maafisa ugavi ambapo amesisitiza wataalam hao wawezeshwa kufika katika vituo hivyo na kupata nafasi ya kufanya ukaguzi katika mifumo mbalimbali ya uedneshaji wa vituo hivyo ili waweze kubaini baadhi ya matatizo ya kimifumo pia.

Katika hatua nyingine Dkt, Gwajima amewataka wakurugenzi wa Halmashauri  kufungua maduka ya dawa jamii katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuongeza hali ya upatikanani wa dawa na mapato.

Wakati huo huo Dkt. Gwajima ameupongeza mkoa wa Simiyu kwa kufanya vizuri katika eneo la ukaguzi na ufuatiliaji jambo ambalo limechangia kuongeza hali ya upatikanaji wa dawa na mapato ya vituo kuongeza hadi mara tano ya mapato ya awali.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa rai kwa Wafamasia mkoani hapa kujitathmini katika utendaji kazi wao ili kuhakikisha kuwa wanadhibiti matumizi ya dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Aidha, Mtaka amesema ni vema viongozi wote katika ngazi ya wilaya na mkoa kuhakikisha anatimiza wajibu wake na katika utoaji wa huduma za afya ndani ya mkoa  ikiwa ni pamoja na kufuatilia taarifa za ukaguzi wa dawa na mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange amesema katika kipindi cha Januari hadi julai 2020 mkoa huu umefanya ukaguzi katika vituo 42 vya huduma

Kati ya vituo 119 kubaini kasoro mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujazaji hafifu wa leja, thamani ya dawa kutoingizwa katika vitabu na kasi ya matukio kukosekana kwa dawa.

Dkt. Dugange  amemeongeza kuwa baada ya ukaguzi huo kumekuwa na udhibiti wa upotevu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi, kuongezeka kwa wateja vituoni  na mapato yameonezeka; ambapo mapato ya mwezi Januari kwa vituo 22 yalikuwa shilingingi 37, 349, 762 kabla ya ukaguzi na kufikia 78,778,964 mwezi Julai baada ya ukaguzi.

Naye Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Mika Mollel amesema ili wakaguzi wa ndani waweze kufanya kazi yao vizuri ni vema wakapewa nafasi ya kuingia katika mifumo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mifumo ya dawa na ukusanyaji wa mapato huku akiomba waaajiri kuwawezesha wakaguzi hao kutekeleza majukumu yao

Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Enock Yakobo ametoa rai kwa Halmashauri zote mkoani Simiyu kuhakikisha kuwa zinakuwa na rekodi sahihi ya dawa na jambo la hali ya upatikanaji wa dawa lijadiliwe katika vikao vya halmashauri na watakaohusika katika upotevu wa dawa na mapato wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:https://simiyuregion.blogspot.com/2020/08/dkt-gwajima-aagiza-mikoa-yote-nchini.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • Naibu Waziri Silinde Aridhishwa Ujenzi wa Bwalo, Madarasa Sekondari ya Anthony Mtaka Busega

    March 06, 2021
  • A NaibuWaziri Silinde Aridhishwa Ujenzi wa Bwalo, Madarasa Sekondari ya Anthony Mtaka Busega

    March 06, 2021
  • Naibu Waziri Silinde Atoa Miezi Miwili Bariadi, Itilima Kukamilisha Mabweni

    March 05, 2021
  • Bilioni 75 Kujenga Kituo Cha Kupozea Umeme Simiyu

    March 04, 2021
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa